ABBAS KUNYO ASEMA HAZINA YA KARO YA WADI YA SHILINGI MILIONI 150 HAITAFUTILIWA MBALI KAUNTI YA TANA RIVER

Waziri wa elimu, Jinsia na Michezo kaunti ya Tana River Abbas Kunyo amesema hazina ya karo ya wadi ya shilingi milioni 150 kwa mwaka haitafutiliwa mbali licha ya kuwepo kwa mchakato wa kuanzisha hazina nyingine ya GOVERNORS SCHOLARSHIP.
Kunyo amesema lengo la hazina ya Gavana inapania kupiga jeki utoaji wa karo kwa wanafunzi ambao wanafanya taaluma mbalimbali kama ya Afya, uhandisi miongoni mwa nyingine.
Muswada huo wa GOVERNOS SCHOLARSHIP uliwasilishwa katika bunge la kaunti ya Tana River mwaka wa 2019 na kukosa kuidhinishwa, huku Abbas Kunyo akidai kuwa wakati wa vikao vya umma sheria hiyo ilipania kuondoa hazina ya karo ya wadi.