KIWANDA CHA MAZIWA CHA KCC ENEO LA MIRITINI KUIMARISHWA

Serikali kupitia wizara ya vyama vya ushirika na biashara nchini inapanga kupanua kiwanda cha maziwa cha KCC eneo la Miritini kaunti ya Mombasa na kukifanya kuwa kiwanda bora cha maziwa.
Haya ni kwa mjibu wa waziri katika wizara hiyo nchini Simon Chelugui akizungumza katika kikao na gavana wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir na kusema tayari mikakati imeanzishwa ili kuanza kukiboresha.
Aidha, amekana madai kuwa kiwanda hicho cha KCC eneo la Miritini kaunti ya Mombasa kimebinafsishwa.
Kwa upande wake Gavana wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir ameahidi kushirikiana na wizara hiyo ili kuhakikisha kila kitu kinatekelezwa vyema na uchumi wa Kaunti ya Mombasa kuimarika hata zaidi.
KIWANDA