MIKAKATI INAENDELEZWA KAUNTI YA LAMU KUBORESHA USALAMA

Naibu Kamishna wa kaunti ya Lamu Charlse Kitheka amesema mikakati thabiti imeanzishwa na asasi za usalama katika kaunti hiyo ili kuongeza maafisa wa ziada, NPR katika sehemu mbalimbali za kaunti ya Lamu ili kusaidiana na wanajeshi wa KDF pamoja na vitengo vingine vya usalama kuimarisha usalama.
Kulingana na Kitheka maafisa hao wa NPR watatumwa kwenye maeneo ambayo yanakabiliwa na ukosefu wa usalama kama sehemu ambazo zinapakana na msitu wa Boni, Hindi, Kiunga, Witu, Mpeketoni na Basuba.
Amesema lengo kuu ni kuhakikisha wanaohusika na visa vya mashambulizi ya mara kwa mara ambavyo vinaaminika kutekelezwa na magaidi wa Al –Shabaab vinadhibitiwa vilivyo.