SAMSON ZIA ASEMA HAKUNA MTU ANAPASWA KULIPA FEDHA ILI KUPEWA BASARI WADI YA ADU.

Mwakilishi wa wadi ya Adu eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi, Samson Zia amesema hakuna mwananchi anayepaswa kulipa ada yoyote ili kupata fedha za ufadhili wa masomo ya watoto wao kupitia basari za serikali za kaunti ama hata ile ya kitaifa.
Zia amesema wameweka mikakati ya kuhakikisha hakuna ambaye, analaghaiwa na baadhi ya wale walioko katika kamati ya hazina ya CDF kwenye wadi hiyo ya Adu.
Akizungumza na wanahabari katika eneo hilo, mwakilishi wa wadi huyo amesema ili kukabiliana na dhana kuwa wapo baadhi ya watu ambao hutozwa kiasi fulani cha fedha, ili watoto wao wapewe basari hizo walichukua hatua ya kuwapatia fursa wananchi kuwachagua wanakamati wanaohisi kuwa wanawafaa.
Vilevile, amesema tayari wamefanya kikao na wanakamati wa hazina ya CDF katika afisi ya mwakilishi wa wa wadi huyo na kuwaonya wanakamati hao dhidi ya kushiriki ufisadi kwa njia yoyote ile.