WANAFUNZI WANAOTOKA KATIKA SHULE ZA MITAA YA MABANDA KAUNTI YA MOMBASA KUNUFAIKA NA UFADHILI WA MASOMO

Ni afueni kwa baadhi ya wanafunzi wanatoka katika shule za mitaa ya mabanda kaunti ya Mombasa baada ya seneta mteule kaunti hiyo Mirajj Abdillahi kuzindua hazina ya ufadhili wa masomo ya masomo ya sekondari kwa wanafunzi hao.
Seneta hiyo amesema kuwa wanafunzi waliopata alama 350 na zaidi ndiyo walengwa wakuu wa mapango huo pamoja na wale walikosa kujiunga na shule za upili za kitaifa kutokana na ukosefu wa karo.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari amesema kuwa wapo baadhi ya wanafunzi waliofanya vyema katika mtihani wa KCPE ila walikosa kubahatika kupata basari za ufadhili wa masomo wa NG-CDF.
Kwa upande wake katibu mkuu wa shule za mabanda APBET Juma Athman Lubambo amempongeza kiongozi huyo huku akitoa wito kwa viongozi wengine kuiga mfano wa kiongozi hao ili kuhakikisha kuwa jamii inaelimika.