Serikali ya kaunti ya Taita Taveta imeanzisha rasmi ujenzi wa kituo cha matibabu ya ugonjwa wa Saratani.
Kulingana na Gavana wa kaunti hiyo Andrew Mwadime, ni kuwa ujenzi wa jumba la kisasa ambalo litatumika kama kituo cha afya cha ugonjwa huo, litajengwa kwa takriban siku 150 na kukamilishwa.
Akizungumza na wananchi katika kaunti hiyo, gavana huyo amesema kuwa idadi kubwa ya wananchi kaunti ya Taita Taveta, wameendelea kupitia changamoto nyingi katika kupata matibabu ya maradhi hayo, jambo ambalo sasa litawapa afueni ya kupata matibabu baada ya jumba hilo kukamilika.
Aidha baadhi ya viongozi katika kaunti hiyo, ametoa wito kwa uongozi wa kaunti ya Taita Taveta kutilia maanani masuala ya afya katika kaunti hiyo.
UJENZI WA KITUO CHA MATIBABU YA UGONJWA WA SARATANI KUANZISHWAKAUNTI YA TAITA TAVETA

