Mjadala kuhusu ulipaji ushuru umeendelea kutawala majukwaa ya kisiasa baina ya serikali ya kenya kwanza na azimio la umoja one kenya huku rais William Ruto sasa akisema ameridhishwa na uamuzi wa Wakenya kuazimia kulipa ushuru.
Akionekana kumjibu mamaNgina Kenyatta baada ya kauli yake kuhusu mdahalo huu mapema wikendi iliopita, Rais Ruto pia ameiagiza halmashauri ya ukasanyaji ushuru KRA kuwapa nafasi wakenya waliojitolea kutekeleza wajibu wao wa ushuru.
Rais Ruto amesisitiza kuwa ni sharti kila mkenya alipe ushuru pasi na kujali tabaka au nafasi yake katika taifa hili, kauli iliyoonekana kulenga familia ya Kenyatta.
Haya yamejiri baada ya kauli ya mama wa kwanza wa taifa Mama ngina Kenyatta kutoa tamko kuhusiana na mijadala inayoendelezwa kuwa familia hiyo inapaswa kuanza kutozwa kodi ili kuongeza ushuru wa taifa hili.
RAIS RUTO ARIDHISHWA NA UAMUZI WA WAKENYA KUAZIMIA KULIPA USHURU

