Wanafunzi wote waliofanya mtihani wa darasa la nane KCPE mwaka uliopita wa 2022 wanatarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza.
Wanafunzi hao wapatao milioni moja watajiunga na shule za sekondari kuanzia hii leo huku idadi ndogo ya wanafunzi hao wakitajwa kufaulu kujiunga na shule ambazo walizichagua huku wengine wakikosa nafasi hizo kufuatia sababu mbalimbali ikiwemo ukosefu wa hela za karo au hata za kugharamia mahitaji ya shule
Hatahivyo serikali imezidi kusisitiza kuwa hakuna mwanafunzi atakayekosa nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza ili kuhakikisha kuwa asilimia 100 ya wanafunzi wanajiunga na shule za upili
Idadi kubwa ya wazazi pia wamelalamikia hali ngumu ya kiuchumi inayochochea wao kushindwa kuwapeleka wanafunzi shule walizoitwa
WANAFUNZI WALIOMALIZA DARASA LA NANE KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA LEO

