MWAKILISHI WA WADI YA MWANAMWINGA EDWARD ZIRO ATOA WITO KWA WAZAZI KUHAKIKISHA WATOTO WAO WANAJIUNGA NA SHULE ZA UPILI

Mwakilishi wa wadi ya Mwanamwinga kaunti ya Kilifi Edward Ziro ametoa wito kwa wazazi ambao watoto wao walimaliza darasa la nane wanajiunga na shule za upili ili kuendeleza masomo yao.
Ziro amesema ni kupitia ushirikiano ndipo watoto wote wataendelea kusoma bila kukabiliwa na changamoto zozote.
Aidha, Edward Ziro ameeleza kusikitishwa na namna vijana wengi katika eneo hilo wanavyositisha masomo yao bila sababu za Msingi.
Akiunga mkono kauli ya Mwakilishi wa wadi hiyo ya Mwanamwinga, Chifu wa eneo hilo Joseph Kapalia amewataka wanafunzi wanaojiunga na shule za upili kuhakikisha wanadumisha nidhamu ili kufanya vyema kwenye masomo yao.