Ni rasmi sasa kinda wa timu ya taifa ya uingereza pamoja na klabu ya Manchester united mwite Mason Greenwood ameondolewa mashtaka yote yanayofungamana na ubakaji yaliyowasilishwa kortini dhidi yake.
Mason Greenwood mwenye umri wa miaka 21 alikamatwa mapema mwaka jana baada ya madai kuibuka kwamba amehusika kwenye shambulio la ubakaji hasa baada ya picha na kanda za video kuchipuka mitandaoni.
Hata hivyo idara ya mashtaka imemwachilia kutokana na mashahidi wakuu wa kesi hiyo kujiondoa.
Ikumbukwe kwamba klabu ya Manchester united baada ya kuchipuka kwa kesi hiyi pamoja na picha zilizofungamana na matukio hayo ilimpiga marufuku ya kutoshiriki mechi yoyote pamoja na kumfungia kutotumia viwanja vyao vya mazoezi.

