WAHALIFU WANAOWATATIZA WAHUDUMU WA BODABODA ENEO LA SHIMBA HILLS WAONYWA

Idara ya usalama eneo bunge la Shimba hills kaunti ya Kwale limewaonya wahalifu wanaotatiza  usalama wa wahudumu wa bodaboda katika baadhi ya maeneo ya eneo bunge Hilo hususan nyakati za usiku.
Akizungumza akiwa eneo la Kizibe naibu kamishna wa eneo bunge hilo Moses Karwigi amesema asasi za usalama zinashika doria pia kuchunguza na kuwasaka wahalifu wanaohusika katika visa hivyo vya mauwaji ya bodaboda maeneo hayo.
Aidha kamishna huyo amewahakikishia wakaazi wa eneo bunge hilo  kuwa usalama utaimarishwa na uchunguzi zaidi unafanywa ili kuwakabili wahusika kisheria.
Kauli yake inajiri  baada ya kuripotiwa visa vya wahudumu wa bodaboda kutoka maeneo hayo kujeruhiwa vibaya.