CONGO BOYS YALENGA KUGEMA TALANTA MASHINANI

Klabu ya Mombasa Congo Boys inalenga kuanza mawindo ya talanta za soka mashinani katika lengo la kuimarisha kikosi chao lakini pia kufanya malezi ya talanta za vijana.

Akizungumza na tama la spoti asubui ya leo Omar Faraj ambaye ni mshauri wa ufundi katika klabu hiyo amesema kwamba Congo Boys itakuwa inafanya zoezi la majaribio ya wachezaji walio kati ya miaka 17-21 katika uwanja wa serani sports ground katika kaunti ya Mombasa kuanzia tarehe 6 hadi 8 mwezi huu.

Kulingana na Faraj ni kwamba kikosi cha Congo Boys kwa sasa kinasubiri uamuzi wa shirikisho la soka la FKF kuhusu hatma ya kuwa ni ligi gani watacheza msimu huu baada ya kushuka kutoka ligi ya daraja la kwanza kitaifa lakini pia msimu jana uliosimamiwa na kamati ya mpito kufutiliwa mbali na shirikisho hilo baada ya kuharamishwa.