Serikali ya kenya imetangaza rasmi mipango ya kujenga makavazi ya kumuenzi bingwa wa riadha za dunia Eliud Kipchoge katika mji wa Eldoret kaunti ya Uasin Gishu.
Kulingana na katibu mkuu wa Wizara ya michezo Ummi Bashir ni kwamba makavazi hayo yatapewa jina la Museum 159 kutokana na ushindi wa kihistoria wa Eliud Kipchoge wa Ineos 159.
Nguli huyo wa dunia anakumbukwa kote ulimwenguni kwa kuwa mwanadamu wa kwanza duniani kumaliza mbio za marathon chini ya kipindi cha masaa mawili.

