MUUNGANO WA WAVUVI ENEO LA MALINDI WAPENDEKEZA KUWEKEWA MATAA

Muungano wa wavuvi wa Mijikenda Fishermen Association katika eneo la Malindi kaunti ya Kilifi, umependekeza kuwekewa mataa katika baadhi ya barabara wanazozitumia kuingia baharini.
Kulingana na Joseph Kaingu mmoja wa wavuvi hao, amesema ukosefu wa mataa katika baadhi ya sehemu hizo, kunahatarisha maisha ya wavuvi hao hasa nyakati za usiku, wakati wanapoendeleza shughuli zao kwenye bahari.
Ni kauli ambayo imeungwa mkono na Salim Mohammed, mmoja wa viongozi wa dini ya Kiislamu ambaye pia ameunga mkono kauli hiyo na kusema iwapo serikali itatekeleza kuweka mataa maeneo ambayo yana giza itakuwa afueni kubwa kwao.
Aidha, mwakilishi wadi ya Shella Twahir Abdulkarim ameitaka serikali kuu kupitia afisi ya mbunge wa Malindi, Amina Mnyazi kushughulikia suala hilo kwa haraka huku akiahidi serikali ya kaunti ya Kilifi kupitia afisi yake, itahakikisha kuwa inakarabati mataa hayo iwapo yatakuwa yameharibika.