Naibu Kamishna wa kaunti ya Mombasa Ronald Mwiwawi amesema vijana wadogo kwenye kaunti wamekuwa wakijihusisha na visa vya Uhalifu.
Kulingana na Mwiwawi Kumechipuka magenge ya kihalifu ambayo yanawahusisha vijana wadogo katika kaunti hiyo hali ambayo amesema inawasababisha kuacha masomo.
Amesema watoto hao ni wenye umri wa miaka 10 hadi 12 na kusema wanapaswa kuwa shuleni na sio kujiunga na magenge ya kihalifu.
Aidha, amesema ni lazima kuwe na ushirikiano thabiti kati ya wenyeji na asasi za usalama ili kuyadhibiti magenge ya kihalifu.
Kauli yake imeungwa mkono na Seneta Mteule Miraj Abdillahi ambaye amesema juhudi zaidi zinapaswa kuongezwa ili kuwarekebisha watoto hao.
VIJANA WENYE UMRI MDOGO KAUNTI YA MOMBASA WANAJIHUSISHA NA VISA VYA UHALIFU

