BUNGE LA KAUNTI YA KILIFI KUTENGA MILIONI MOJA KILA WADI ILI KUIMARISHA MICHEZO

Bunge la kaunti ya kilifi limepitisha mswada wa kutenga bajeti ya shilingi milioni moja kila wadi ili kusaidia kuimarisha michezo kupitia kuwawezesha wachezaji.

Rashid Odhiambo ambaye ni mwakilishi wadi wa mji wa Malindi amesema kwamba changamoto ya usafiri ndio jambo ambalo sasa wanalenga kulikabili katika awamu ya pili kwa kutenga bajeti ambapo wanalenga kununua mabasi ya kusafirisha wachezaji katika kila wadi za kaunti ya Kilifi.

Vilabu vingi vya kaunti ya Kilifi vimekuwa vikilalamikia ukata wa kifedha na usafiri ambao huwalemaza katika harakati za kutafuta mafanikio ya kupanda daraja katika ligi mbali mbali za mashinani.