NAIBU GAVANA WA TAITA TAVETA CHRISTINE KILALO AWATAKA WAZAZI KUWAJIBIKIA MAJUKUMU IPASAVYO

Naibu Gavana kaunti ya Taita Taveta Christine Kilalo amewataka wazazi katika kaunti hiyo kuwafunza watoto wao kuhusu namna ya kutumia simu za mikononi ili kuwadhibiti dhidi ya kupotoka kimaadili.
Kilalo amesema iwapo hilo litatiliwa maanani hakutakuwa na watoto katika jamii ambao wamepotoka kimaadili.
Amesema watoto wengi wamepotoka kimaadili kupitia kutazama video na picha zilizoko kwenye mitandao ya kijamii .
Vilevile, amewahimiza wazazi kuwa karibu na watoto wao na sio kutelekeza majukumu yao ya ulezi ili kuwaandalia maisha mema ya baadae.