Gavana wa kaunti ya Tana River Dhadho Godhana amezilaumu baadhi ya jamii zilizoko kwenye kaunti hiyo kutokana na kile ambacho anadai kuendelea kuzingatia tamaduni ambazo zinaathiri shughuli za maendeleo kaunti ya Tana River.
Amesema hulka ya jamii hizo kuendeleza mila na tamaduni hizo ambazo hazina msingi wowote zimechangia kwa baadhi wenyeji kupinga miradi ambayo inatekelezwa na serikali.
Akitolea mfano wa mradi wa vijiji vya kisasa Gavana Godhana amesema baadhi ya jamii zinadinda kukubali kuhamia maeneo ambayo yametengewa mradi huo.
Gavana huyo amethibitisha kufanya mazungumzo na wazee wa vijiji ili kutupilia mbali baadhi ya sheria za kijamii ili kuruhusu maendeleo na kuwahimiza viongozi wa dini kuingilia ili kufanikisha hilo.
GAVANA WA TANA RIVER AZILAUMU BAADHI YA JAMII KAUNTI YA TANA RIVER

