Mkurugenzi mkuu wa shirika la kutetea haki za kibinadamu la Haki Afrika kaunti ya Mombasa Hussein Khalid amesema sheria inapaswa kuzingatiwa vilivyo katika kuwakabili wahalifu nchini.
Hussein amesema ni sharti sheria zilizobuniwa nchini kuzingatiwa licha ya kuwa taifa la Kenya linashuhudia visa vya uhalifu.
Amesema haifai kwa maafisa wa usalama kutumia nguvu kupita kiasi wanapokabiliana na wahalifu nchini.
Aidha, amesema licha mashirika ya kutetea haki za kibinadamu yanaunga mkono harakati za kukabiliana na utovu wa usalama nchini, asasi za usalama zinapaswa kuzingatia sheria wakati wa kuwakabili wahalifu.
Ni kauli ambayo imeungwa mkono na Zaina Kombo ambaye ni afisa wa shirika la Amnesty International na kuitaka serikali kuchukua hatua za kuzisaidia familia kuwatafuta wapendwa wao ambao walipotea katika mazingira tatanishi nchini.
HAKI AFRIKA YAZITAKA ASASI ZA USALAMA KUWAKABILI WAHALIFU BILA KUWAHANGAISHA

