ENGIN FIRAT AREJEA HARAMBEE STARS

Shirikisho la soka nchini Kenya jana lilithibitisha kwamba Engin Firat atarejea kuchukua majukumu ya kuongoza kikosi cha Harambe stars baada ya mkataba wake wa awali wa muda mfupi kutamatika.

Katika muda mfupi akiongoza timu hiyo ya taifa ya Kenya Engin Firat alipoteza mechi zote mbili za kipindi hicho na hii ilikuwa dhidi ya Rwanda lakini pia Uganda.

Sasa amepewa mkataba wa miaka mitatu na atakuwa mkufunzi atakayepeleka timu ya taifa katika mashindano ya kombe la Afcon mwaka 2026. Mkufunzi huyo anatarajiwa kutua nchini mwezi ujao.