WITO WATOLEWA KWA VIONGOZI WA KILIFI KUTENGA BAJETI YA MICHEZO

Wito umetolewa kwa wawakilishi wadi wa kaunti ya kilifi kupeleka miswada bungeni ambayo itasaidia katika kuimarisha michezo.

Tom Lango ambaye ni mwenyekiti wa fkf tawi la eneo bunge la Malindi ameshauri serikali ya kaunti hiyo kutenga bajeti itakayosaidia kusimamia fedha za kuendesha ligi za mashinani ikizingatiwa kwamba kwa sasa vilabu vingi vinapitia wakati mgumu kifedha.

Wakati hayo yakijiri shirikisho la soka la magarini linalenga kuandaa kikao na wakuu wa vilabu kuanza mikakati ya kujitayarisha kwa msimu mpya wa 2022/2023 katika eneo bunge hilo.

Kulingana na waraka uliotiwa sahihi na katibu mkuu Emmanuel Kazungu ni kwamba mkutano utafanyika kanisani Apostolic Mjanaheri siku ya Jumamosi.