BAADHI YA MABAHARIA ENEO LA SHELLA MJINI MALINDI WAENDELELEA KUHANGAIKA

Licha ya jamii eneo la Shella mjini Malindi kaunti ya Kilifi kuchangia pakubwa katika upatikanaji wa ushuru wa kitaifa kupitia kwa raslimali za baharini, baadhi ya mabaharia eneo hilo la Shella wameendelea kupitia changamoto nyingi katika maisha yao.

Haya ni kwa mujibu wa mwakilishi wa wadi ya Shella mjini Malindi kaunti ya Kilifi, Twahir Abdulkarim ambaye amesema anapania kuwasilisha musuada bungeni utakaopendekeza kiasi cha fedha kinachopaswa kusalia katika wadi hiyo baada ya ushuru huo kukusanywa na serikali ya kitaifa.

Kiongozi huyo ameeleza kuwa hatua hiyo itasaidia kuboresha maisha ya wananchi na hata shughuli ambazo huendelea katika fuo za bahari kaunti ya Kilifi na PWani kwa jumla.

Aidha amesema ipo haja ya jamii kupewa jukumu la kuchunguza utendakazi wa baadhi ya maafisa wa shirika la huduma kwa wanyamapori KWS eneo

la Malindi na kupendekeza hatua ya wao kuhamishwa iwapo hawasaidii jamii.