Katibu wa muungano wa walimu KUPPET kaunti ya KIlifi, Risper Awinja amemtaja aliyekuwa Waziri wa elimu nchini Prof. George Magoha kama kiongozi ambaye alichangia kwa asilimia kubwa kuboresha sekta ya elimu nchini.
Risper ambaye ameeleza kusikitishwa na Kifo cha Magoha ambacho kilitokea jana Jioni kutokana na kile kinachosemekana kusababishwa na Mshtuko wa moyo, amesema Magoha alitekeleza wajibu wake katika kuhakikisha hakuna visa vya udanganyifu vinashuhudiwa kwenye mitihani ya kitaifa.
Akizungumza na lulu Fm amesema licha ya kuwa Magoha ameaga dunia, juhudi zake katika kuimarisha viwango vya elimu nchini zitasalia kukumbukwa na wengi.
Aidha, amesema misimamo yake thabiti katika utendakazi wake ilichangia kwa viwango vya elimu kuimarika nchini licha kuna baadhi ya walimu pamoja na wadau mbalimbali wa elimu walikuwa wakikosoa misimamo yake.

