IDARA YA ELIMU TAITA TAVETA YASEMA ITAHAKIKISHA WANAFUNZI WOTE WALIOMALIZA DARASA LA 8 WANAJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA

Mkurugenzi mkuu wa idara ya elimu eneo bunge la Taveta kaunti ya Taita Taveta Hassan Abdulraman amesema watahakikisha wanafunzi wote ambao walimaliza masomo ya darasa la 8 mwaka jana wa 2022 wanajiunga na shule za upili mwaka huu wa 2023.
Kulingana na Hassan kila mtoto ana haki ya kusoma na kuwataka wazazi kwenye eneo hilo kuhakikisha watoto wao wanajiunga na kidato cha kwanza.
Aidha, amesema ufadhili wa fedha za basari kutoka kwa hazina ya NG – CDF kwa sasa unatolewa kwa wanafunzi wa kidato cha pili hadi wale wa vyuo vikuu.