BADI TWALIB AIPONGEZA SERIKALI KUU

Mbunge wa Jomvu kaunti ya Mombasa Badi Twalib ameipongeza serikali kuu kupitia wizara ya uchukuzi, kwa kuweka saini mkataba wa ujenzi wa barabara kuu ya Jomvu Mariakani.
Kulingana na Badi ni kuwa huenda ujenzi wa barabara hiyo ukaanza kutekelezwa hivi karibuni, jambo ambalo litasaidia kurahisisha shughuli za usafiri na maendeleo ya jamii eneo bunge hilo.
Badi ambaye ni kiongozi wa mrengo wa Azimio la Umoja One Kenya, amesema kuwa atashirikiana na serikali ya Rais William Ruto, katika kuhakikisha kuwa analeta maendeleo kwa wakaazi wa eneo bunge lake na kaunti ya Mombasa kwa Jumla.
Wakati ou huo amempongeza Rais Kwa kumteua Mohamed Daghar, kuwa katibu wa kudumu katika wizara ya uchukuzi nchini huku akimtaka katibu huyo kuweka juhudi zaidi katika kutekekeza wajibu wake kwa jamii na taifa la Kenya kwa jumla.