Afisa msimamizi wa kituo cha usambazaji maji cha Kambicha, Magarini kaunti ya Kilifi Rajab Kazungu amesisitiza haja ya serikali ya kaunti ya Kilifi kukiwezesha kifedha kituo hicho.
Kazungu amesema kuwa hatua hiyo itawawezesha kugharamia ada za nguvu za umeme sawia na kulipa wafanyikazi kwenye kituo hicho mbali na kuboresha huduma za usambazaji maji katika eneo hilo.
Afisa huyo amesema kuwa tatizo la uhaba wa maji katika maeneo hayo yataweza kukabiliwa iwapo wito huo utazingatiwa.
Aidha Kazungu amesema wanapania kubuni mradi ambao utasaidia katika kukuza kituo hicho cha usambazaji maji kifedha.
Wakati uo huo, Kazungu ameitaka serikali ya kaunti ya kilifi kuwasaidia kukarabati baadhi ya mabomba ya maji yanayopasuka mara kwa mara hali itakayorahisha utoaji na usambazaji wa huduma za maji kwa wakaazi.
WITO WATOLEWA KWA SERIKALI YA KAUNTI YA KILIFI KIKIWEZESHA KIFEDHA KITUO CHA KUSAMBAZA MAJI YA KAMBICHA

