HIMIZO LATOLEWA KWA WATU WA KWALE KUTOKUTENGANA KWA MISINGI YA DINI

Kiongozi wa vijana katika kaunti ya Kwale, Hafswa Mohamed amesisitiza haja ya wakaazi kujumuika na kushirikiana pasipo kutengana kwa misingi ya kidini.

Hafswa amesema baadhi ya dhana potovu zilizopo katika dini huchangia mgawanyiko baina ya wakaazi kwani kupitia dhana hizo utengano hudhihirika miongoni mwa wanajamii.

Kiongozi huyo amesema kuwa viongozi wa dini pia wanapaswa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha inakabiliana utengano wa kidini katika jamii.

Hafswa amesema wanajamii wanapaswa kukubaliana kuwa dini hazipaswi kuwa kigezo cha utengano wao ila waungane licha ya kuwa kwenye dini na imani mbalimbali.