Mbunge wa LungaLunga kaunti ya Kwale Mangale Munga Chiforomodo amewataka maafisa wa hazina ya ustawi wa maeneo bunge NG-CDF kutojihusisha na ufisadi wakati wa utoaji fedha za basari kwa wanafunzi wanaolengwa.
Akizungumza eneo la Dzombo kwenye eneo bunge hilo wakati wa uzinduzi wa basari, Chiforomodo amesema maafisa ambao huitisha hongo kutoka kwa wazazi kabla ya kuwahudumia watakabiliwa vikali kisheria.
Mbunge huyo amesema fedha za basari kwa sasa zimeongezwa kutoka shilingi milioni 35 hadi milioni 60 kwa lengo la kufaidi wanafunzi zaidi ya elfu 5 wa shule za kutwa na elfu mbili wa shule za mabweni na vyuo vikuu.
Ni hatua iliyoungwa mkono na wenyeji wa eneo bunge hilo wakisema watapunguziwa mzigo wa kusaka karo ikizingatiwa kwamba tayari gharama ya maisha iko juu mno.
MAAFISA WA HAZINA YA NG-CDF ENEO LA LUNGA LUNGA KAUNTI YA KWALE WAONYWA

