Jumla ya wanafunzi 16 waliokamilisha darasa la 8 mwaka jana kaunti ya Kwale ni miongoni mwa wanafunzi 1000 nchini waliofaidika na ufadhili wa masomo ya WINGS TO FLY kutoka kwa benki ya Equity mwaka huu wa 2023.
Kulingana na Jacob Akida ambaye mkurugenzi wa benki hiyo tawi la kaunti ya Kwale amesema wanafunzi hao waliopata zaidi ya alama 350 wanatoka katika familia zisizojiweza kifedha.
Amewataka wazazi ambao watoto wao wamefaidika na mradi huo kuwapatia ushauri nasaha wanapojiandaa kujiunga na shule za upili ili kuwaepusha dhidi ya kushawishika na kujihusisha na mambo maovu ambayo huendaa yakaathiri masomo yao.
Wanafunzi hao wanatajumuika na wanafunzi wengine waliopata ufadhili huo nchini Kenya ili kupata ushauri nasaha kuhusiana na maswala ya elimu kwa muda wa siku 3 katika shule ya upili ya wasichana ya kitaifa ya Pangani.
JUMLA YA WANAFUNZI 16 WALIOKAMILISHA DARASA LA 8 KAUNTI YA KWALE KUNUFAIKA NA UFADHILI WA MASOMO YA WINGS TO FLY

