Mbunge wa Jomvu kaunti ya Mombasa Badi Twalib anataka nafasi za ajira katika miradi mbalimbali kwenye serikali kuu zipatiwe kwanza vijana wa eneo bunge hilo.
Kulingana na Twalib lazima vijana wa eneo bunge hilo wapewe kipaumbele kwenye masuala ya ajira ili waweze kujiendeleza kimaisha.
Amesema miradi kama wa Dongo Kundu na wa Reli ya Kisasa ya SGR kutoka Miritini hadi katikati mwa mji wa Mombasa inapaswa kupewa vijana wa eneo bunge hilo la Jomvu ili kuwaepusha dhidi ya kujiunga na kujiunga na magenge ya kihalifu au hata kujihusisha na utumizi wa dawa za dawa za kulevya.
Vilevile, Badi Twalib amesema ataweka juhudi zaidi kuhakikisha vijana wenye ujuzi wanapata stakabadhi zao ili kuweza kujiendeleza kimaisha badala ya kusalia mitaani.
BADI TWALIB ATAKA NAFASI ZA KAZI KUTOKA SERIKALI KUU KUPEWA KWANZA VIJANA WA JOMVU

