KAUNTI YA LAMU INAKABILIWA NA CHANGAMOTO ZA KIFEDHA ZA KUFADHILI WANAFUNZI

Naibu gavana wa kaunti ya Lamu Raphael Munyua amesema serikali ya kaunti hiyo inakabiliwa na changamoto za kifedha za kufadhili wanafunzi katika kaunti hiyo.
Munyua amesema changamoto hiyo imechangiwa na mabadiliko ya kalenda ya elimu nchini tangu mwaka wa 2020 wakati wa janga la Virusi vya Corona nchini.
Aidha, amesema serikali ya kaunti ya Lamu inaweka mikakati ya kupata mwafaka wa changamoto hiyo.

Vilevile, amemtaka Seneta wa kaunti ya Lamu Joseph Githuku kuwasilisha musuada bungeni wa kuiongezea kaunti hiyo mgao wa fedha.