Arsenal sasa itakutana na Manchester city katika hatua ya 16 katika michuano ya FA baada ya kusajili ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya klabu ya Oxford.
Katika mechi ya jana washika mtutu hao wa London walipeana mafunzo ya kutosha kwenye soka kwa Oxford kupitia bao la Mohamed Elneny pamoja na mabao mawili kinda wa uingereza Eddie Nketia.
Mechi ya Manchester City na Arsenal ya kombe la FA hatua ya 16 bora itachezwa tarehe 28 mwezi huu wa Januari.

