Viongozi wa eneo bunge la Malindi kaunti ya Kilifi wameahidi kuboresha uchumi wa raslimali za baharini, katika eneo bunge la Malindi hasa kwenye wadi ya Shella mjini Malindi kaunti ya Kilifi.
Kwa mujibu wa mbunge wa eneo la Malindi kaunti ya Kilifi, Amina Mnyazi wadi ya Shella ndiyo ambayo inaathirika moja kwa moja na masuala uchumi wa raslimali za baharini na hivyo basi ipo haja ya mikakati zaidi kuwekwa ili kuboresha shughuli za kibiasha katika eneo hilo.
Kiongozi huyo amesema kuwa kwa sasa wanaendeleza mazungumo ya kuhakikisha kuwa misuada mbali mbali kuhusiana na suala hilo yanafikishwa katika bunge la kitaifa pamoja na lile la kaunti hii ya Kilifi ili kujadiliwa na hata kutekelezwa.
Vilevile mbunge huyo ameeleza matumaini ya suala hilo kuafikiwa kwa urahisi kwani yupo katika kamati ya bunge la kitaifa, inayohusiana na masuala ya uchumi wa raslimali za baharini yaani Blue Economy huku mwakilishi wa wadi ya Shella Twahir Abdulkarim pia akiwa mmoja wa wanakamati hiyo katika bunge la kaunti ya KIlifi.
UCHUMI WA MALINDI KAUNTI YA KILIFI KUIMARISHWA

