MKUFUNZI RIMBA WA BOSUSTER APONGEZA FKF KWA MIPANGO MIZURI YA LIGI YA MSIMU UJAO

Mkufunzi wa Bosuster fc klabu ambayo inashikilia ubingwa wa shindano la soka la Haki Yetu eneo bunge la Magarini Kaunti ya Kilifi bwana Kenedy Rimba anasema kikosi chake kiko imara kwa msimu ujao wa ligi ya magarini msimu wa 2022/2023 msimu ambayo unatarajiwa kuanza rasmi majuma mawili yajayo.

Rimba ambaye vijana wake wametinga fainali za mashindano ya mbunge wa magarini Harry Kombe amesisitiza kwamba analenga uwa na matokeo mazuri katika ligi hiyo baada ya kufanya usajili na marekebisho katika kikosi chake.

Mkufunzi huyo pia amepongeza hatua ya uongozi wa fkf eneo bunge la magarini kwa kuafiki kuzigawanya timu kulingana na wadi za eneo hilo ili kupunguza mzigo kwa vilabu hasa vilabu vinavyoandamwa na changamoto ya ukata wa kifedha.