ZOEZI LA UPIGAJI KURA LINAENDELEA KATIKA WADI YA SHELLA KISIWANI LAMU

Zoezi la upigaji kura linaendelea katika wadi ya Shella kaunti ya Lamu baada ya kung’oa nanga leo mwendo wa saa kumi na mbili asubuhi.
Wenyeji wa wadi ya Shella wanapiga kura kumchagua mwakilishi wa wadi mwingine baada ya kujiuzulu kwa Azhar Ali Mbarak ambaye kwa sasa ni spika wa bunge la kaunti ya Lamu.
Wadi hiyo yenye takribani wapiga kura 3,632 imewavutia jumla ya wawaniaji wanne kwenye wadhifa huo mmoja wao akiwa mwanamke.
Kuna jumla ya vituo 9 vya kupigia kura.