MAAFISA WA KWS NA WENYEJI WA TAITA TAVETA WAHIMIZWA KUKABILIANA NA UHASAMA WA MARA KWA MARA

Wito wa ushirikiano umetolewa baina ya maafisa wa shirika la huduma kwa wanyamapori KWS na wakaazi wa kaunti ya Taita Taveta kwa minajili ya kukabiliana na uhasama wa mara kwa mara kati ya wakaazi na wanyamapori.
Kwa mujibu wa wakaazi wa maeneo mbalimbali ya kaunti hiyo wakiwemo wale wa Kishushe, kaunti ndogo ya Wundanyi wamesema kuwa wamekuwa wakikadiria hasara kutokana na uvamizi wa wanyamapori ambao huwatekelezea uharibifu wa mimea yao.
Wakaazi hao wamesema kuwa wanyama hao wa porini wamekuwa wakiwapelekea kukumbwa na baa la njaa kwani wanakosa chakula kinachoishia kuharibiwa kikiwa mashambani.
Kufuatia hilo, mwakilishi wadi maalum Anisa Omar amesema kuna haja ya viongozi wa serikali, viongozi wa KWS na wakaazi wa kaunti hiyo kushirikiana katika kusaka suluhu la kudumu dhidi ya swala hilo tata la uvamizi wa wanyamapori.