LIGI YA FKF MAGHARINI KUREJEA RASMI WIKI MBILI ZIJAZO

Ligi mbali mbali za soka la fkf nchini Kenya zinaendelea kurejea pole pole na eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi linatarajia kuanza rasmi msimu wa 2022/2023 katika kipindi cha wiki mbili zijazo.

Kwa sasa kuligana na uongozi wa ligi ya fkf tawi la Magarini ni kwamba ligi hiyo imevutia vilabu vingi vya mashinani na sasa huenda kukawa na makundi manne kutoka maeneo mbali mbali ya eneo bunge hilo.

Kiongozi huyo wa soka anasema kwamba wachezaji wa mashinani wanafaa kujitayarisha kwa mazuri mengi kutoka kwa serikali kuu akipongeza hatua ya serikali kulenga kufanya mradi wa kusaka soka mashinani kupitia mashindano ya Bottom Up Tournament akisema kwamba mradi huo huenda ukaboesha zaidi soka la Kenya kuanzia mashinani mpaka ngazi ya kitaifa.