KENYA YAORODHESHWA NAFASI YA 22 KATIKA VIWANGO VYA CAF

Taifa la Kenya sasa limeorodheshwa nafasi ya 22 katika viwango vya soka barani Afrika.

Hii ni kutokana na taarifa iliyochapishwa na shirikisho la soka la Afrika Caf na hii ndio ya punde zaidi.

Haya yanajiri baada ya Kenya kufungiwa kwa kipindi cha takriban mwaka mmoja kutokana na serikali kuingilia masuala ya soka ya shirikisho la FKF.

Hata hivyo hali ya soka la Kenya sasa imerudi shwari baada ya serikali mpya kuingia uongozini na wziri mpya ababu namwamba kuchukua usukani wa wizara hiyo ya vijana pamoja na talanta na michezo.