Mkufunzi wa zamani wa klabu ya chelsea Avram Grant sasa amepewa kazi ya kuwa mkufunzi mkuu wa timu ya taifa ya Zambia.
Mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 67 sasa anatarajiwa kuipeleka Zambia katika anga za ushindani wa ubingwa wa afrika baada ya kuonekana kuwa na uzoefu ikizingatiwa kwamba amekuwa mkufunzi mkuu wa timu ya taifa ya Ghana pamoja na kuwa mkufunzi katika klabu ya westham nchini Uingereza.
Kibarua chake cha kwanza ni kuiongoza Zambia kupata tikiti ya kucheza katika mashindano ya afcon baada ya taifa hilo kukosa kufuzu kwa mashindano matatu mfululizo.
Ni mkufunzi ambaye anakumbukwa sana kwa kuipeleka Ghana katika fainali za Afcon mwaka 2015 ambapo walipoteza kwa ivory coast kupitia mikwaju ya penanlti.

