SHULE YA MSINGI YA BANDACHO ENEO BUNGE LA MAGARINI KAUNTI YA KILIFI YAANDIKISHA MATOKEO BORA ZAIDI YA KCPE.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Bandacho kaunti ndogo ya Magarini kaunti hii ya Kilifi, Constance Kanze ameeleza furaha yake baada ya shule hiyo, kuandikisha matokeo bora katika mtihani wa kitaifa wa KCPE.

Katika mazungumzo ya kipekee na meza yetu ya habari, mwalimu huyo amesema kuwa jumla ya wanafunzi 17, walipata alama 400 na zaidi kati ya wanafunzi 99 waliofanya mtihani wa KCPE na kuandikisha jumla ya alama 375.31.

Wakati huo huo, ametaja uhaba wa walimu kama changomoto kubwa inayokumba shule hiyo huku akiitaka serikali, kupitia wizara ya elimu kuongeza walimu katika shule za umma, ili kuboresha elimu katika shule hizo.

Kwa upande wao wanafunzi walioongozwa katika shule hiyo Maxwell Kizito aliyepata alama 421 na Jeniffer Kadzo Hinzano, aliyepata alama 416, wameeleza baadhi ya changamoto walizopitia ikiwemo uhaba wa maji, pamoja ukame.

Aidha KAUNTI za Kwale na Kilifi zimetajawa kufanya vyema katika matokeo ya mtihani wa huo wa kitaifa ukanda huu wa Pwani, huku Shule nyingi za kibinafsi zikifanya vyema zaidi ikilinganishwa na zile za serikali.