BUNGE LA KAUNTI YA TANA RIVER LA TENGA MGAO WA KUKABILIANA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA.

Jumla ya shilingi milioni hamsini zimetengwa na serikali ya kaunti ya Tana River, ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya anga.

Akizungumza na wananchi katika eneo hilo, afisa wa mazimgira George Kasi ameelezea kuwa hatua hiyo imejiri baada ya bunge hilo, kuidhinisha sheria itakayo tumika katika kutekeleza suala hilo.

Amesema kuwa uongozi wa kaunti hiyo, umekubaliana kufunga baadhi ya mito ya maji ya chumvi, inayo elekeza maji yake katika mto Tana, pamoja na kuanzisha miradi ya upanzi wa miti ya mikoko.

Kwa upande wake katibu mkuu wa idara ya serikali inayohusika na ustawishaji wa maeneo kame nchini Idris Dokuta, amewahimiza wanajamii eneo hilo kukumbatia upanzi wa miti ya mikoko, ili kukuza uchumi wa bahari kaunti hiyo.