Rais William Ruto amesema kuwa serikali yake itajitahidi kuhakikisha kuwa inapiga vita ufisadi katika idara na afisi mbali mbali za serikali.
Akizungumza katika kikao na makamishna wa kaunti zote 47 nchini, Rais amewahakikishia wakuu hao wa idara ya usalama, kuwa kama kiongozi wa taifa, atahakikisha wananchi wananufaika na huduma na misaada mbali mbali, inayotolewa na serikali kwa malengo ya mwananchi mashinani.
Amesema kuwa ipo haja ya wakuu hao wa idara ya usalama katika kaunti za taifa hili, kushirikiana na serikali kuu katika kuhakikisha kuwa wanafanikisha suala hilo.
Vile vile kiongozi wa taifa amesema makamishana wa kaunti, wanajukumu la kuhakikisha kuwa viongozi wa idara hiyo ya usalama mashinani, wanahamasishwa kuhusiana na umuhimu wa wananchi kushiriki katika zoezi la upanzi wa miti, katika sehemu hitajika ili kusisitiza hilo kwa jamii.

