AFISA WA DCI AFIKISHWA MAHAKAMANI KAUNTI YA KILIFI KWA MADAI YA UBAKAJI.

Afisa wa polisi wa kitengo cha DCI kaunti ndogo ya Magarini kaunti ya Kilifi amefikishwa mbele ya mahakama ya Kilifi kwa shutma za kumnajisi mtoto katika eneo hilo.

Afisa huyo kwa jina George Nangoye amekana mashtaka matatu mbele ya hakimu mkuu mkaazi Geofrey Kimang’a.

Mashtaka hayo yanajumuisha kosa la kumnajisi msichana wa miaka 16 mnamo mwezi wa tisa mwaka 2021,kosa la kutumia wadhfa wake wa kikazi kumnajisi mtoto aliyekuwa chini ya ulinzi wake.

Afisa huyo ametajwa kumnajisi msichana huyo katika eneo la Marereni.
Ametozwa faini ya dhamana ya shilingi laki mbili na mdhamini wa kiasi sawa na hicho au fedha taslimu elfu 40.