KARIM BENZEMA ASTAFU SOKA LA KITAIFA

Karim Benzema mshambuliaji wa klabu ya real Madrid amethibitisha kwamba amestafu soka la kitaifa baada ya fainali za siku ya jumapili ambapo Ufaransa walipoteza kwa Argentina kupitia mikwaju ya penalti.

Benzema alikosekana katika mechi za kombe la dunia katika makala ya 22 kutokana na jeraha. Katika takwimu zake za uchezaji akivalia uzi wa ufaransa amefunga mabao 37 katika mechi 97.

Mwezi October Benzema alishinda taji la ballon dor na amekuwa akitamani saana kushiri mashindano ya kombe la dunia baada ya mwaka 2018 kuachwa nje kutokana na kiwango chake cha mchezo kipindi hicho ambapo Ufaransa walitangazwa mabingwa.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *