NICK SALAT ATAKIWA KUTOJIBIZANA NA GIDEON MOI

Chama cha KANU (Kenya African National Union) tawi la kaunti ya Kilifi, kimetoa wito kwa katibu mkuu wa  kitaifa wa chama hicho Nick Salat, ambaye pia alikabidhiwa barua ya kubanduliwa mamlakani siku chache zilizopita, kutojibizana na mwenyekiti wao Gideon Moi.
Kulingana na katibu mkuu wa chama hicho  Alex Mwanza, amemtaka  Salat kufuata maagizo ya  Moi  na kubaki nje ya ofisi,  akisubiri hatma yake baada ya kikao na kamati ya nidhamu.
Akizungumza katika afisi za  chama cha KANU mjini Kilifi, Mwanza amemkosoa  Salat kwa madai ya kutotaka kukosolewa na kiongozi wa chama hicho na kusema kuwa ni ishara utovu wa nidhamu.
Wakati huo huo Mwanza amesema  wanaheshimu uamuzi wa baraza la NEC,  na kusema kuwa Salat anapaswa kutilia maanani maagizo yote atakayo pewa na baraza hilo.
Ikumbukwe kwa kinara wa chama hicho Gideon Moi aliandikia barua ya kumsimamisha Salat, kuendelea kuhudumu kama katibu mkuu wa chama cha KANU  mnamo Desemba 15 mwaka huu.