Nguli wa Brazil mwite Pele anaendelea kupata afueni wiki mbili baada ya kuanza matibabu katika hospitali moja mjini Sao Paulo. Kulingana na madaktari na wauguzi wanaomhudumia wanasema kwamba haijabainika lini ataruhusiwa kwenda nyumbani baada ya matibabu ya ugonjwa wa mapafu uliokuwa umemkabili katika siku za hivi punde.
Pele mwenye umri wa miaka 82 ambaye pia anatambulika kama legendari katika soka la dunia kwa kushinda mataji matatu ya kombe la dunia amekuwa akikabiliwa na ugonjwa wa saratani pamoja na maumivu ya kufanyiwa upasuaji kutolewa uvimbe katika utumbo wake, zoezi ambalo lilifanyika mwezi September.
Sogora huyo ambaye ni mfungaji wa mabao zaidi ya elfu moja katika maisha yake ya soka la ushindani amekuwa akitumiwa jumbe za kumtakia afueni ya haraka na wanasoka ikiwemo taifa wenyeji wa mashindano ya kombe la dunia Qatar ambao walikuwa wakichapisha jumbe nyingi kumtia moyo Pele.

