Afisi ya mbunge wa Malindi kaunti ya Kilifi Amina Mnyazi, imetangaza kuwepo kwa nafasi elfu moja za ufadhili wa masomo ya kozi mbalimbali za kibiashara kupitia mitandao.
Kulingana na mbunge huyo kuna umuhimu mkubwa kwa wananchi katika eneo la Malindi kaunti ya Kilifi, kuthamini masomo hayo kupitia kwa mitandaoili kuboresha viwango vya elimu eneo bunge la Malindi.
Akizunguza na wanahabari mjini Malindi kaunti ya Kilifi, Mnyazi ameeleza kuwa wale watakaojiunga na mpango huo wa elimu, watalazimika kulipa kiasi Fulani cha fedha, kitakachosaidia kulipia ada za kimitandao wakatakayokuwa wakitumia.
Aidha, amesema tayari wamebaini baadhi vya taasisi za elimu zitakazokuwa zikitumika katika kuendeleza masomo hayo katika kila wadi ya eneo bunge la Malindi, ili kuhakikisha kila wananchi ananufaika na mpango huo.
MBUNGE WA MALINDI AMINA MNYAZI ATANGAZA NAFASI ZA UFADHILI WA MASOMO

