Mbunge wa Lamu Mashariki kaunti ya Lamu, Ruweida Obo ameishinikiza serikali ya kitaifa kwa ushirikiano na serikali ya kaunti kuweka lami kwenye barabara ya Mthangawanda – kizingitini katika kisiwa cha Pate.
Obo amesema kuwa eneo hilo limesalia nyuma kimaendeleo kutokana na kukosa miundo msingi muhimu jambo lililochochea shikizo hizo.
Mbunge huyo aidha amemhimiza gavana wa kaunti ya Lamu kuwekeza zaidi katika maeneo ya Lamu mashariki sambamba na ule uwekezaji wa hali ya juu wa miundo msingi uliotekelezwa Lamu magharibi.
Obo amesisitiza haja ya eneo bunge la Lamu mashariki kuimarishwa kwa minajili ya kuwanufaisha wakaazi wa eneo hilo.
RUWEIDA OBO AISHINIKIZA SERIKALI KUU KWA USHIRIKIANO NA YA KAUNTI YA KILIFI KUWEKA LAMI BARABARA YA MTANGAWANDA – KIZINGITINI

