Naibu kamishna wa eneo bunge la Malindi kaunti ya Kilifi, Thuo Ngugi amewaonya wamiliki wa mabaa na mikahawa katika eneo hili la Malindi dhidi ya kuendeleza kelele nyakati za usiku, msimu huu wa sherehe za krismasi.
Kulingana na Ngugi idadi kubwa ya wamiliki wa sehemu hizo za burudani, wamekuwa wakitatiza amani ya baadhi ya wananchi wanaoishi katika sehemu hizo jambo ambalo amedai kutokuwa la haki kwa wananchi wengine wanaoishi karibu na sehemu hizo.
Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Jamhuri hapa mjini Malindi katika uwanja wa Cleopatra, Ngugi ameahidi kuanzisha msako dhidi ya mabaa yatakoyokuwa yakipiga mziki wa sauti ya juu na kuhakikisha kuwa anafuatilia hadi kwa afisi ya gavana wa kaunti ya Kilifi, Gideon Mung’aro ili kuona kwamba wamiliki wa maeneo hayo ya burudani yanawajibishwa kisheria kuwa.
Kwa upande wake mbunge wa Malindi, Amina Laura Mnyazi amewataka wazazi kuwalinda wanao, dhidi ya kupachikwa ujauzito msimu huu wa sherehe za krismasi na kuhakikisha kuwa wanafahamu sehemu ambazo watakuwa wakitumia muda wao mwingi wakati huu wanapokuwa majumbani.
WAMILIKI WA MABAA NA MIKAHAWA MJINI MALINDI WAONYWA

