Gavana wa Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir amewaonya wafanyibiashara wote wa miraa kaunti ya mombasa kuhakikisha kuwa hawafanyibiashara hizo karibu na taasisi za kielimu.
Akizungumza katika sherehe za Jamhuri kwenye bustani ya Mamangina kaunti hiyo ya Mombasa Nassir amesema vijana wengi wenye umri mdogo wameishia kuwa waraibu wa bidhaa hiyo licha ya kuwa wao bado ni wanafunzi.
Wakati huo huo Nassir ametoa onyo dhidi ya watu wanaojenga majumba kiholela bila ya idhini kutoka kwa serikali na idara husika akisema kuwa hawatasazwa na mkono wa sheria.
Kwa upande wake kamishna wa Mombasa John Otieno ameeleza kugadhabishwa na idadi chache cha wakaazi wanaohudhuria sherehe za kitaifa ikiwemo hii ya leo ya Jamhuri.
WAFANYABIASHARA WA MIRAA KAUNTI YA MOMBASA WAONYWA

